
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MJI wa Serikali wa Mtumba, jijini Dodoma, unatarajiwa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali kupitia ukaribu wa ofisi za wizara na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi katika eneo hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Nsubili Joshua, alisema hayo Oktoba 29, 2026, alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea jengo la wizara hiyo, kuelekea uzinduzi wa majengo ya Serikali na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba.
Alisema uwepo wa mazingira bora ya kazi na miundombinu ya pamoja unawawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi, huku ukaribu wa taasisi ukirahisisha uratibu wa shughuli za Serikali na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Alieleza kuwa awali Serikali ilikabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji kutokana na viongozi na watumishi kusafiri mara kwa mara kati ya Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya mikutano na shughuli mbalimbali za kikazi.
“Kuwepo kwa taasisi za Serikali katika eneo moja kunasaidia kupunguza gharama za safari za kikazi, mikutano na uratibu wa shughuli mbalimbali za Serikali,” alisema.
Aliongeza kuwa mpangilio huo pia unaimarisha uwazi na uwajibikaji kwa kurahisisha ufuatiliaji wa utekelezaji wa maamuzi, mipango na maelekezo ya Serikali.
Uzinduzi wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba ulioziozinduliwa Oktoba 30, 2026.







