Serikali kubadili kilimo cha kujikimu kuwa cha kibiashara

Sarah Moses, Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara.

 Amesema kuwa mabadiliko hayo yanafanyika kwa kuzingatia malengo ya kitaifa kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo 2015 -2025, Sera ya Kilimo ya Mwaka 2013 na Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2021-2025. 

Hayo ameyasema julai 2 mwaka huu katika maonesho ya 15 ya  nanenane  kanda ya kati ambapo alisema kuwa juhudi hizi za Serikali, zinatarajiwa kusaidia wakulima kuanzisha Viwanda vidogo vya kusindika mazao ya kilimo na Mifugo ili kuyaongezea thamani kabla ya kuingizwa sokoni.

Amesema kuwa kwakuwa ni rahisi kwa Serikali kusaidia wazalishaji wakiwa kwenye vikundi ushirika au umoja, hivyo anawataka  wazalishaji kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupewa ruzuku au mikopo yenye riba nafuu ambayo itasaidia kuboresha shughuli za uzalishaji na hivyo kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.”


“Utaratibu huu wa maonyesho unatoa fursa kwa wananchi wanaotembelea mabanda ya maonesho kujifunza mbinu na teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji bora kutoka kwa wakulima na wafugaji wenzao, Taasisi za Kitafiti, bodi za mazao na mashirika mbalimbali ya umma na watu binafsi. Hivyo, nawapongeza sana wote mliojiandaa na kujitolea kushiriki katika maonesho haya yenye mafunzo mengi “amesema Senyamule.

3 thoughts on “Serikali kubadili kilimo cha kujikimu kuwa cha kibiashara

  1. Rasimu Na. 1

    WBLM NA. …… WA MWAKA 2020/20

    MUHTASARI WA WARAKA

    KICHWA CHA WARAKA

    Mapendekezo ya Kutunga Sheria ya kuanzisha Wakala wa Carrot Tanzania 2020. (The Institutional Establishment Act, 2011).

    WAZIRI ANAYEWASILISHA Waziri wa Viwanda na Biashara.

    MUHTASARI WA MAPENDEKEZO Baraza la Mawaziri litoe maamuzi ya msingi ya kuanzisha Wakala wa Carrot Tanzania ya Mwaka 2020.

    CHIMBUKO LA WARAKA Changamoto zilizojitokeza katika kusimamia kilimo cha Carrot Tanzania kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji nchini.

    MAMBO MUHIMU YATAKAYOZINGATIWA Kuongeza viwango vya usimamiaji (management) katika shughuli za za uzalishaji wa Carrot nchini na kupunguza uwezekano wa kutokea tatizo la Njaa nchini; Kubadilisha Mamlaka ya utoaji vibali na leseni za mashamba yatakayotumika kuzarisha zao hilo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara; Kuweka utaratibu wa usimamizi wa Kemikali zinazotumika kama malighafi katika uzalishaji wa zao hilo; Kuweka utaratibu wa kuwarasimisha kwa kuwaunganisha na kutoa ajira za kudumu kwa wakulima na wazalishaji wa Carrot kwa kushirikisha mapendekezo ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa; Kuwepo kwa utaratibu wa fidia kwa wananchi watakaothibitika kupata madhara yatokanayo na mahitaji ya shughuli za uzalishaji wa zao hilo; na Kuweka utaratibu utakaoanzisha mfumo wa ki – elektroniki wa kuhifadhi takwimu za uzalishaji wa zao hilo nchini.

    MATOKEO YA SHERIA Kupungua au kudhibiti matumizi haramu ya ardhi katika uzalishaji wa zao hilo pamoja na vifaa vyake ikiwemo tractors; Kupunguza gharama za uzalishaji wa kilimo cha Carrot nchini, kupunguza gharama za bei ya bidhaa nchini, Kuimarika kwa usalama katika utunzaji, umilikaji, usafirishaji, ununuzi, uuzaji na utumiaji wa Carrot nchini; Kuongezeka kwa mapato ya Serikali yatokanayo na shughuli za uzalishaji wa Carrot; kuhamasisha shughuliza uhifadhi, elimu, kupack na masoko bidhaa ya bidhaa hiyo na kuwepo kwa mfumo rasmi wa ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za uzalishaji wa Carrot

    MAHITAJI YA RASILIMALI Jumla ya Shilingi 60,924,500 fedha za ndani na shilingi 70,000,000 fedha za nje zimetengwa katika Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya Mwaka 2020/21 kwa ajili ya uanzishawaji wa wakala kwa ajili ya Mishahara, elimu pamoja na majukumu mengine ya Wizara.

    USHIRIKISHWAJI WA WADAU Wakati wa kuandaa Waraka, maoni ya wadau mbalimbali yamepatikana kutoka: Wizara za nchi Ofisi ya Rais, (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora); Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira; Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu; Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Katiba na Sheria; Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; Wizara ya Mifugo na Uvuvi;na Wakulima wadogo wadogo wa Carrot ambao wataajiliwa na Wakala

    RATIBA YA UTEKELEZAJIBaada ya Waraka huu kukubaliwa, Rasimu ya Sheria husika itaandaliwa Mwezi Januari, 2021 na kuwasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuandaa muswada.

    W-M A.J.M.K.

    XXXXXXXXXXX

    hapa naona kama marais wote hawakupoteza muda

    jk – kilimo uti wa mgongo (wakasahau bar, kilabu, ugonjwa, nyumba nao ulikuwa uti wa mgongo kwa wengine)

    mwinyi (ruksa fanya utakavyo ili tujue uti wa mgongo wako)

    mkapa (kuplant those inspiration)

    jakaya (kilimo kwanza full kununua matrector labda saizi yatakuwa kama VX full services kila week)

    magufuli (hapa kazi tu labda watategeneza kazi)

    ajaye baibai kwa sabau ya steel mnaharibu

    XXXXXXX

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *