Dkt. Mpango amrithi Warioba uongozi SUA

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), akichukua nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, aliyemaliza muda wake.

Uteuzi huo ni miongoni mwa uteuzi wa viongozi watano uliofanywa na Rais Samia, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 17,2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Mbali na Dkt. Mpango, Rais Samia alimteua Ezekiel Mathias Goboro kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Katika uteuzi mwingine, Rais amemteua Talha Mohamed Waziri kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo, Waziri alikuwa Msaidizi wa Rais, Diplomasia.

Aidha, Lucas Aaron Mayanga na Dkt. Miraji Ukuti Ussi wameteuliwa kuwa Mabalozi na watapangiwa vituo vya kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *