Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha

WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.07-1024x643 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, leo Oktoba 3, 2026, ameongoza kikao cha Kamati Tendaji ya IPU kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Arusha, Tanzania, Oktoba 5-9, 2026.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na unatarajiwa kuhudhuriwa na takribani washiriki 2,000 kutoka mabunge 183 wanachama wa IPU, wakiwemo Maspika, Wabunge, Makatibu wa Mabunge na maafisa mbalimbali kutoka mabunge duniani.

WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.08-1024x682 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha
WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.08-1-1024x673 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha
WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.08-2-1024x670 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha
WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.09-1024x682 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha
WhatsApp-Image-2026-10-03-at-05.19.07-1-1024x621 Dkt Tulia aongoza Kamati Tendaji ya IPU kuelekea Mkutano Mkuu Arusha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *