Yanga yapoteza mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho Afrika.

Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Afrika kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wamefungwa nyumbani magoli mawili kwa moja katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho uliochezwa Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam dhidi Waalgeria USM Alger.

Yanga walianza kufungwa dakika ya 32 kupitia kwa Aimen Mahious kabla ya Yanga kusawazisha kipindi cha pili kwa goli la kinara wa magoli wa mashindano hayo, Fiston Mayele aliyefunda dakika ya 82 kabla ya kufungwa goli la pili dakika ya 86 kupitia kwa Islam Merili.

Yanga watajiuliza na kujaribu kushinda ubingwa huo wa kombe la Shirikisho kwenye mchezo wa marudiano wa fainali hapo Juni 03, 2023 kule Algeria.

One thought on “Yanga yapoteza mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *