Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho

WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.49.57-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Ruto CGH, amewasili nchini Tanzania kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku Mbili, Mei 4-5, 2026.

Ruto amepokelewa kwa gwaride la heshima na kupokelewa na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Thabit Mahamod Kombo.

Aidha, Ruto atakutana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam ambapo pia watafanya mazungumzo ya wawili ili kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.

Mapema kesho, Mei 5, 2026, Ruto atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kabla ya kuhitimisha ziara yake.

WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.49.56-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.49.55-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.49.58-1024x650 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.50.00-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.50.01-1-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.50.02-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho
WhatsApp-Image-2026-05-04-at-04.50.03-1024x683 Rais Ruto awasili Tanzania, kulihutubia Bunge kesho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *