DIB yajivunia kupunguza migogoro Sekta ya Fedha

Na Salha Mohamed

odi ya Bima ya Amana (DIB), imesema imefanikiwa kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika uendeshaji wa taasisi za kifedha nchini kupitia utekelezaji wa majukumu yake ya kulinda amana za wateja.

Hayo yalisemwa Julai 2, 2026 na Ofisa Mwandamizi wa DIB, Joyce Shala, wakati Waziri wa Fedha, Balozi Dkt. Khamis Mussa Omar, alipotembelea banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa.

Shala amesema DIB imefanikiwa kuwalipa wateja wa iliyokuwa Benki ya FBME kwa asilimia 85, ambapo katika awamu ya kwanza walilipwa asilimia 35, awamu ya pili asilimia 28 na awamu ya tatu asilimia 35.

Katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha amepokelewa na viongozi pamoja na wafanyakazi wa DIB na kupatiwa maelezo kuhusu majukumu ya bodi hiyo, huduma inazotoa pamoja na jitihada zinazoendelea kufanywa katika kutoa elimu kwa umma kuhusu Mfumo wa Bima ya Amana.

Aidha, Balozi Dkt. Khamis Mussa Omar amepata fursa ya kufahamu mchango wa DIB katika kulinda amana za wateja wa benki na taasisi za fedha, sambamba na kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha nchini.

2-5-1024x576 DIB yajivunia kupunguza migogoro Sekta ya Fedha

Katika hatua nyingine Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Rahma Salim Mahfoudh, amewataka wananchi kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kujifunza kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi za umma na binafsi, ikiwemo elimu ya Mfumo wa Bima ya Amana inayotolewa na Bodi ya Bima ya Amana (DIB).

Katika ziara yake kwenye banda la DIB, alipokelewa na viongozi na wafanyakazi wa DIB ambao walimpa maelezo kuhusu majukumu ya bodi hiyo, huduma inazotoa pamoja na jitihada za kutoa elimu kwa umma kuhusu Mfumo wa Bima ya Amana.

Aidha, amepata fursa ya kufahamu mchango wa DIB katika kulinda amana za wateja wa benki na taasisi za fedha pamoja na kuimarisha uthabiti wa sekta ya fedha nchini.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Dkt. Mahfoudh alisema maonesho hayo ni fursa muhimu kwa wananchi kujionea huduma, bidhaa, ubunifu na teknolojia mbalimbali zinazotolewa na washiriki.

“Ninawahimiza wananchi kutumia fursa hii kutembelea maonesho haya ili kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa taasisi na kampuni zinazoshiriki. Hapa kuna huduma, bidhaa, ubunifu na teknolojia zinazoweza kuongeza uelewa wao na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi katika shughuli zao za kila siku,” amesema.

3-6-768x1024 DIB yajivunia kupunguza migogoro Sekta ya Fedha

Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa DIB, Shala, amesema ushiriki wa bodi hiyo katika Sabasaba 2026 unalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya DIB katika kulinda amana za wateja wa benki na taasisi za fedha pamoja na umuhimu wa Mfumo wa Bima ya Amana katika kuimarisha utulivu na imani katika sekta ya fedha.

Shala amewataka wananchi kutembelea banda la DIB ili kupata elimu kuhusu huduma na majukumu ya bodi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *