Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi

IMG-20261115-WA0000-1024x683 Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi

Na Benny Mwaipaja, Antalya-Uturuki

Maofisa wa Serikali ya Tanzania, wataalam wa fedha na washirika wa maendeleo wamekutana Antalya, Uturuki, katika Mkutano wa COP 31 pembezoni wakati wa Siku ya Biashara na Fedha ya mikutano ya COP31 ya mwaka 2026, kujadili upatikanajii wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi nchini Tanzania.

Majadiliano yalisisitiza hatari kubwa za kiuchumi zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na hatua za kimkakati ambazo taifa linafanya ili kupata ufadhili unaohitajika.

Vida Malle, anayewakilisha Wizara ya Fedha, amebainisha ukubwa wa changamoto hiyo, akisema kuwa mabadiliko ya tabianchi yanatarajiwa kupunguza ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa asilimia 2.15 kufikia mwaka 2050 na yanaweza kuwaingiza takriban watu milioni 2.6 katika umaskini.

Ili kufikia utekelezaji wa michango iliyopangwa kitaifa (National Determined Contributions- NDCs 2.0 ) ya nchi kufikia mwaka 2030, Tanzania inahitaji dola bilioni 19.2. Kukiwa na dola bilioni 7 zilizopatikana tayari, taifa linakabiliwa na pengo la ufadhili la dola bilioni 12

Pamoja na Mipango ya Kitaifa ya Kustahimili Mabadiliko ya Tabianchi (National Adaptation Plans-NAPs), jumla ya mahitaji ya rasilimali zinahitajika hadi karibu dola bilioni 40 ifikapo 2035.

Anaendelea kueleza umuhimu wa uwasilishaji wa ripoti za uendelevu katika sekta za umma na binafsi, kwa msisitizo wa pekee kwa rasilimali za kifedha zilizokusanywa na matumizi yaliyotengwa kwa ajili ya Mabadiliko ya Tabianchi

Kushughulikia hilo, Wizara ya Fedha imeanzisha Kitengo Maalum ya Uratibu wa Fedha za Mabadiliko ya Tabianchi ambayo ina jukumu la kwenda zaidi ya vyanzo vya kawaida vya ufadhili kama misaada na Mikopo nafuu ili kuchunguza mbinu mbadala za kifedha, ikiwemo hatifungani za kijani, hatifungani za bluu na fedha za kaboni.

Lengo kuu la majadiliano pia imesisitizwa umuhimi wa Uwekaji Alama kwenye Bajeti za mabadiliko ya Tabianchi mfumo ulioelezwa na Bi. Tunsume Mlawa kwamba kwa kutumia msimbo maalum wa bajeti, serikali sasa inaweza kufuatilia kiasi kinachotengwa na kinachotumika kwa shughuli zinazohusiana na hali ya hewa katika sekta zote, badala ya kudhani kuwa ni wizara ya mazingira pekee inayoshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Derick Kiwia, kutoka Taasisi ya UmFinancial Sector Deepening Trust-FSDT), inayofanya kazi Tanzania kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na makundi yaliyokuwa yameachwa pembeni kama wanawake, vijana na wakulima wadogo, alisisitiza umuhimu wa data na utafiti katika mchakato huu.

Amebainisha kuwa taasisi yake inashirikiana na Climate Policy Initiative kutayarisha ripoti ya kwanza kabisa ya ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania.

Utafiti huo unalenga kufuatilia mtiririko wa fedha, kutambua vyombo vinavyotumika na kubaini nakisi ili kuhakikisha kuwa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinaendana na malengo ya kitaifa.

Aidha, mkutano huo uliangazia uzoefu kutoka kwa washirika wa ukanda ambapo Bw. Dennis Mugagga, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Mabadiliko ya Tabianchi katika Wizara ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Kiuchumi ya Uganda, alisisitiza umuhimu wa umiliki wa kitaifa.

Ameshauri kuwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ziinapaswa kuongoza ajenda zao za fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuzipatanisha na matarajio ya ukuaji wa kitaifa badala ya kutegemea washirika wa nje pekee.

Pia amesisitiza kuwa uwekaji alama wa bajeti ya mabadiliko ya tabia nchi (budget tracking) ni mchakato endelevu unaohitaji mafunzo ya mara kwa mara na utaalam wa ndani ya nchi.

Kwa mtazamo wa mbele, Wizara ya Fedha inatarajia kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Fedha za Mabadiliko ya Tabianchi na Uainishaji wa Fedha Endelevu.
Mipango hii inatarajiwa kutoa mfumo mmoja wa kukusanya rasilimali, kuandaa miradi inayoweza kufadhilika na kushirikisha sekta binafsi, ambayo inatarajiwa kuchukua jukumu kubwa katika maono ya maendeleo ya nchi kupitia Dira 2050.

Wizara ya Fedha inatoa wito wa ushirikiano kutoka kwa washirika mbalimbali ikiwemo Washirika wa Maendeleo, Taasisi za Kifedha, Sekta Binafsi, wadau wa serikali na wasio wa serikali ili kufanikisha matarajio haya.

IMG-20261115-WA0002-1024x683 Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi
IMG-20261114-WA0002-1-1024x683 Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi
IMG-20261114-WA0001-1024x683 Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi
IMG-20261115-WA0002-1-1024x683 Tanzania Yapanga Njia ya Kuziba Pengo la Mabilioni ya Fedha Kukabiliana na Mabadiliko Tabianchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *