Songwe yafungua milango kwa Sekta Binafsi kwenye miradi

Na Mwandishi Wetu, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabir Makame, amepigia chapuo matumizi ya mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama njia kuu na endelevu ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kukuza uzalishaji wa kiuchumi mkoani humo.

Makame ametoa msimamo huo wakati akihutubia katika Jukwaa la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Songwe Dira 2050 Forum) lililofanyika mkoani Songwe.

Jukwaa hilo lenye lengo la kuweka mikakati ya kiuchumi ya Mkoa kutekeleza Dira ya maendeleo 2050 mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Akiwasilisha maono ya Mkoa huo, Makame alibainisha kuwa mkoa wa Songwe una fursa kubwa za kijiografia, kilimo, madini na biashara ya mipakani, ambazo haziwezi kuendelezwa kwa kutegemea bajeti ya serikali pekee.

Pia alieleza kuwa njia pekee ya kuleta mapinduzi ya haraka bila kuwaumiza wananchi ni kukaribisha sekta binafsi kuwekeza kupitia ubia wa PPP kwenye ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji, masoko ya kisasa, na viwanda vidogo na vya kati.

2-1 Songwe yafungua milango kwa Sekta Binafsi kwenye miradi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *