Rais wa zamani wa Guinea-Bissau ahudhuria Tamasha la Kizimkazi

WhatsApp-Image-2026-08-14-at-03.23.02 Rais wa zamani wa Guinea-Bissau ahudhuria Tamasha la Kizimkazi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Aliyekuwa Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, amehudhuria kilele cha Tamasha la Kizimkazi 2026 visiwani Zanzibar, akiwa mgeni maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Embaló ameshiriki katika hafla ya kilele cha tamasha hilo inayofanyika katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, ikiwakutanisha wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Tamasha la Kizimkazi 2026, lenye kaulimbiu “Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa,” lilianza Agosti 12 na linafikia kilele leo, Agosti 14, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mgeni rasmi.

WhatsApp-Image-2026-08-14-at-03.23.03 Rais wa zamani wa Guinea-Bissau ahudhuria Tamasha la Kizimkazi
WhatsApp-Image-2026-08-14-at-03.23.03-1-1024x677 Rais wa zamani wa Guinea-Bissau ahudhuria Tamasha la Kizimkazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *