DC Mpogolo: Wakandarasi wasio na uwezo wasiombe kazi Ilala

Na Salha Mohamed

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wakandarasi wanaotaka kuomba zabuni za ujenzi katika wilaya hiyo kuhakikisha wana uwezo wa kutekeleza kazi wanazoomba.

Mpogolo ametoa kauli hiyo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kimanga–Mazda yenye urefu wa meta 400, inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.7 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

2-4-1024x682 DC Mpogolo: Wakandarasi wasio na uwezo wasiombe kazi Ilala

Amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga shilingi bilioni 14 kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa barabara mbalimbali ndani ya jiji hilo, jambo ambalo litawavutia wakandarasi wengi kuomba zabuni za utekelezaji wa miradi hiyo.

“Najua kwa kiasi hiki cha fedha wakandarasi wengi watatamani kuja kuomba kazi hapa kwetu Ilala, lakini hatutawavumilia wakandarasi wasiokuwa na uwezo. Kama huna uwezo, usije kuomba kazi hapa,” alisisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

3-4-1024x682 DC Mpogolo: Wakandarasi wasio na uwezo wasiombe kazi Ilala

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi mzawa, Kampuni ya Osaka Construction Ltd, ni kiungo muhimu kati ya Wilaya za Ilala na Ubungo.

Awali, eneo hilo lilikuwa likikumbwa na changamoto na kutopitika, hususan wakati wa mvua.

4-4-1024x683 DC Mpogolo: Wakandarasi wasio na uwezo wasiombe kazi Ilala
5-3-1024x682 DC Mpogolo: Wakandarasi wasio na uwezo wasiombe kazi Ilala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *