Chuo cha DMI, DMU wasaini makubaliano ya ushirikiano

Dalian, China

CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Bahari cha Dalian Maritime (DMU) cha nchini China lengo la makubaliano hayo ni kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya elimu ya bahari.

Mkuu wa chuo cha DMI, Prof. Tumaini Gurumo, amesema ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizo mbili na kueleza mafanikio ambayo yatapatikana kupitia mahusiano hayo kwa miaka mingi ni pamoja na kubalishana uwezo kwa wanafunzi pia kupeana uzowefu kwa watumishi wa vyuo hivyo.

2-1-1024x684 Chuo cha DMI, DMU wasaini makubaliano ya ushirikiano

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha DMU, Prof. Shan Hongjun alieleza dhamira ya Dalian Maritime University ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya taasisi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano katika maendeleo ya elimu ya bahari, utafiti na ubunifu.

Ameongeza kuwa mahusiano haya ni kielelezo cha mahusiano mazuri baina ya Uchina na Tanzania.

Makubaliano hayo yalisainiwa tarehe Juni 4, mwaka huu katika kampasi ya chuo hicho jijini Dalian nchini China, baada kutia saini Mkuu wa chuo cha DMU amesema makubaliano hayo yatakayowezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za pamoja zikiwemo kubadilishana wanafunzi na wahadhiri, kufanya tafiti za pamoja za kisayansi, kuandaa programu za pamoja za kitaaluma, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika maandalizi ya mitaala na mafunzo ya kitaalamu yanayokidhi mahitaji ya sekta ya usafirishaji majini.

3-1-1024x678 Chuo cha DMI, DMU wasaini makubaliano ya ushirikiano

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni mwanzo mpya katika kuanzisha na kutekeleza miradi ya pamoja yenye ubora wa hali ya juu kwa kutumia rasilimali za kielimu zilizopo katika taasisi zote mbili pia itasaidia kuongeza uwezo wa wahadhiri na wanafunzi, kuimarisha tafiti za pamoja na kuendeleza matumizi ya teknolojia na ubunifu katika sekta ya bahari.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya elimu ya bahari, utafiti, ubunifu na utekelezaji wa ajenda ya Uchumi wa Buluu nchini Tanzania na China, huku yakifungua fursa mpya za ushirikiano wa kimataifa kwa wanafunzi na watumishi wa taasisi hizo.

4-2-1024x684 Chuo cha DMI, DMU wasaini makubaliano ya ushirikiano
5-1-1024x683 Chuo cha DMI, DMU wasaini makubaliano ya ushirikiano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *