Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL

-Ndejembi Aahidi Kuunga Mkono Mpira wa Kikapu Nchini

WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.32.05-1024x819 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TIMU ya Dar City imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) baada ya kuifunga Stein Warriors vikapu 66-50 katika fainali iliyochezwa usiku wa Jumapili, Oktoba 18, 2026, kwenye Uwanja wa IST, Masaki.

Fainali hiyo imeshuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ambaye alimkabidhi kombe nahodha wa Dar City baada ya mchezo. James Amotre aliibuka mchezaji nyota wa fainali hiyo na kuisaidia timu yake kumaliza msimu ikiwa kileleni.

Akizungumza baada ya mchezo, Ndejembi ameipongeza Dar City na Stein Warriors kwa kiwango walichoonesha, akisema Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo na kuunga mkono maendeleo ya sekta hiyo.

Amesema mpira wa kikapu unaendelea kuvutia vijana wengi na unaweza kuwa chanzo cha ajira na kipato kupitia vipaji vyao. Aliwataka wasanii na wafanyabiashara kujitokeza kudhamini timu za kikapu ili kuongeza ushindani wa ligi hiyo.

Makamu huyo wa Rais pia ameeleza kufurahishwa na ushiriki wa timu za wanawake katika ligi hiyo, akisema unaonesha kukua kwa mchezo wa kikapu nchini.

Katika hatua nyingine, Ndejembi amekubali ombi la kuwa mlezi wa mpira wa kikapu nchini lililotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Makonda amesema Serikali inalenga kuboresha miundombinu ya michezo na burudani, ikiwemo kujenga uwanja wa kisasa wa ndani (Arena) utakaotumika kwa shughuli mbalimbali.

Fainali hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso; Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA; Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, pamoja na wasanii, watu maarufu na wananchi.

WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.21.00-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.59-1024x836 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.58-1-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.58-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.57-1024x641 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.54-1-1024x641 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.56-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.56-1-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.54-2-1024x683 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL
WhatsApp-Image-2026-10-18-at-14.20.54-1024x819 Dar City Yatwaa Ubungwa wa BDL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *