
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amezihamasisha Taasisi za Dini nchini kuwa daraja la amani kwa kushirikiana na Serikali ili kuimarisha mahusiano mema, mshikamano na umoja wa kitaifa.
Sangu ameyasema hayo leo, Oktoba 18, 2026, jijini Dar es Salaam, alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu John Jumanne Wambura wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Aidha, amesema Falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayohusu Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Ujenzi Mpya inapaswa kuendelezwa kama sehemu ya utamaduni wa Taifa, huku akizitaka taasisi za dini kuendelea kuhimiza upendo, kuheshimiana, mazungumzo na utatuzi


