SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli

IMG-20261014-WA0047-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli

Na Mwandoshi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, amesema vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) nchini vina mtaji unaozidi Sh trilioni 1.7, ambao unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi endapo utaelekezwa zaidi katika shughuli za uzalishaji, ikiwamo kilimo, mifugo na biashara.

Mweli amesema fedha hizo ni fursa muhimu ya kuongeza uzalishaji, kupanua biashara na kuimarisha uchumi wa wananchi, hususan kwa kuwapatia wakulima, wafugaji na wajasiriamali mitaji yenye masharti nafuu.

Akizungumza katika chakula cha jioni kilichoandaliwa wakati wa Kongamano la 26 la Kimataifa la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Barani Afrika (SACCA), amesema kongamano hilo limetoa fursa kwa washiriki kujadili mbinu bora za kuimarisha uendeshaji wa SACCOS, kuongeza mitaji na kuelekeza fedha katika shughuli zenye tija kiuchumi.

Amesema ni muhimu kuhakikisha fedha zinazokusanywa na SACCOS zinatumika kikamilifu kufadhili sekta za uzalishaji zinazohitaji mitaji, badala ya kubaki bila kuleta mchango unaostahili katika kukuza shughuli za kiuchumi.

Mweli amesema Serikali, kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na jumuiya za SACCOS nchini, inaendelea kuimarisha uhusiano kati ya vyama hivyo na vyama vingine vya ushirika vinavyojishughulisha na uzalishaji.

Ameeleza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuunganisha SACCOS na vyama vya wakulima, wafugaji na wazalishaji wengine, ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji na kupanua masoko ya bidhaa zao.

Kuhusu manufaa ya kongamano hilo, Mweli amesema linatoa nafasi ya kubadilishana uzoefu, kujenga mitandao ya ushirikiano kati ya SACCOS za Tanzania na nchi nyingine za Afrika, pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara na wawekezaji kutafuta fursa za kushirikiana na vyama hivyo.

Ameongeza kuwa kongamano hilo ni fursa kwa Tanzania kuonesha uwezo wake wa kuandaa mikutano ya kimataifa na kuimarisha uhusiano na mataifa mengine kupitia sekta ya ushirika.

IMG-20261014-WA0045-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli

Vijana, wanawake kupewa kipaumbele

Katika hatua nyingine, Mweli amesema matumizi ya mifumo rafiki ya kidijitali ni muhimu katika kuwavutia vijana kujiunga na vyama vya ushirika na kushiriki katika shughuli za kilimo na uzalishaji.

Amesema vijana wanahitaji mifumo inayorahisisha usajili na upatikanaji wa huduma za ushirika kwa njia za kidijitali, sambamba na elimu itakayowawezesha kuelewa manufaa ya kujiunga na vyama hivyo.

Amebainisha kuwa ni muhimu kuwaonesha vijana namna wanavyoweza kujipatia kipato na kujenga maisha bora kupitia kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji zinazofanywa kwa mfumo wa ushirika.

Aidha, amezitaka taasisi za Serikali na vyombo vya habari kushirikiana katika kutoa elimu kwa vijana kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mipango ya kuwawezesha kupata mitaji kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara zao.

Kwa mujibu wa Mweli, ushirikiano huo utasaidia kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za uzalishaji, kuwawezesha kunufaika na fursa za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa.

IMG-20261014-WA0042-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0037-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0035-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0035-1-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0032-1-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0028-1-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli
IMG-20261014-WA0018-1024x683 SACCOS Zinamtaji wa Sh. Tril. 1.7 Unaoweza Kuchochea Uchumi-Mweli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *