TASHICO kukamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba Julai

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

WAZIRI wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema Serikali kupitia Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) inatarajia kukamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba mwishoni mwa Julai 2026, hatua itakayorejesha huduma muhimu za usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika

Prof. Mbarawa amesema hayo mkoani hapa baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa meli hiyo, ambapo alibainisha kuwa mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 33 umefikia asilimia 90 ya utekelezaji na kueleza kuwa kazi zilizobaki ni pamoja na kuipandisha meli kwenye chelezo kwa ajili ya ukaguzi wa sehemu za chini ya maji pamoja na kutoa na kufunga upya shafti ya meli

2-16-1024x683 TASHICO kukamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba Julai

Aidha, amesema majaribio ya meli yanatarajiwa kuanza katikati ya mwezi Julai ili kubaini na kurekebisha changamoto zozote zinazoweza kujitokeza kabla ya kuanza rasmi kutoa huduma

“Tunatambua umuhimu wa MV Liemba kwa wananchi wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa pamoja na wadau wengine wa usafiri katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika Serikali imejipanga kuhakikisha meli hii inaanza kufanya kazi rasmi kabla ya mwisho wa mwezi Julai mwaka huu,” amesema Prof. Mbarawa

Ameongeza kukamilika kwa ukarabati huo kutaimarisha usalama wa usafiri majini kutokana na maboresho yaliyofanyika katika mifumo ya umeme, mawasiliano na vifaa vingine muhimu vya uendeshaji wa meli

3-13-1024x683 TASHICO kukamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba Julai

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ukarabati wa MV Liemba, Mhandisi Ernest John, amesema kuwa kazi za ukarabati zinaendelea vizuri na zinazingatia viwango vya kitaalamu, huku majaribio ya awali ya meli yakitarajiwa kufanyika Julai 17 na 18, 2026.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutarejesha uwezo wa MV Liemba kutoa huduma kwa ufanisi zaidi na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wanaotegemea usafiri wa majini katika maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika

4-11-1024x683 TASHICO kukamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba Julai

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *