
Waziri wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi, amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, leo Juni 29, 2026.
Akiwa mkoani Tanga, Waziri Ndejembi ametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwamo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika eneo la Chongoleani, Tanga, unaolenga kusafirisha mafuta ghafi yaliyogunduliwa nchini Uganda kwenda kwenye masoko ya kimataifa.
Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi ameambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.








