Waandishi wa habari 18 wapenya kuwania tuzo za EJAT msimu wa 16

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAANDISHI wa Habari 18 wamefanikiwa kufikia hatua ya uteuzi katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) msimu wa 16, baada ya majaji kutumia mfumo mpya wa kidigitali kuchambua jumla ya kazi 594 zilizowasilishwa kutoka makundi 11 ya tuzo.


‎Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Mwenyekiti wa Kamati ya Waandaaji wa EJAT 16, Ernest Sungura, imeeleza hayo leo Mei 20, 2026 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Amesema kuwa mfumo huo mpya umeingizwa kwa mara ya kwanza, na kuleta mabadiliko makubwa katika mchakato wa uteuzi. Mfumo huo unahakikisha uchujaji wa kazi kidigitali, tathmini bila upendeleo, na kuzingatia ushahidi wa athari za kazi za waandishi kwa jamii.
‎
‎“Matumizi ya mfumo huu yamesaidia kupunguza idadi ya wateule kutoka wastani wa watu 30 hadi 35 wa mwaka uliopita hadi 18 pekee mwaka huu, hatua inayoongeza ushindani na kuimarisha ubora wa kazi zilizowasilishwa,” amesema Sungura.
‎
‎Matokeo rasmi ya washindi wa kila tuzo yanatarajiwa kutangazwa Mei 29, 2026 katika hafla maalum itakayofanyika jijini Dar es Salaam. Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jaji Nestor Kayobera, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
‎
‎Wateule waliotajwa mwaka huu ni:
‎Shaban Hamisi (Nipashe), Simon Mkina (Pambazuko Online), Daniel Samson (Nukta Africa), Diki Kanyika (Sahara Media), Mackriner Siyovelwa (Crown Digital), Esau Ng’umbi (Nukta Africa), Sanula Athanas (Nipashe), Abel Kilumbu (EATV), Francis Kajubi (The Guardian), Devotha Kihwelu (Mwananchi), Vitus Medard (The Guardian), Anthony Rwekaza (Watetezi Online TV), Neema Abel (The Guardian), Isack Lukumay (Orkonerei FM), Joseph Kirati (The Chanzo), Kelvin Makwinya (Nukta Africa), Abdallah Kurwa (ITV) na Huwaida Moh’d (Assalaam FM).
‎
‎Tuzo za EJAT zinaendelea kuwa jukwaa muhimu la kutambua vipaji vya uandishi wa habari nchini, zikichangia kukuza ubora, uwajibikaji na athari chanya za vyombo vya habari kwa jamii

EASUNN-780x470-1 Waandishi wa habari 18 wapenya kuwania tuzo za EJAT msimu wa 16

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *