Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72

Na Mwandishi Wetu, Tanga

UJENZI wa Daraja la Pangani mkoani Tanga umefikia asilimia 72 ya utekelezaji wake, huku kazi zikiendelea katika hatua ya ujenzi wa sehemu ya juu ya daraja hilo.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tanga, Mhandisi Msama Kosani Msama, amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa Daraja la Pangani pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa jumla ya kilomita 25.6 katika kipande cha barabara ya Pangani–Tungamaa.

Screenshot_20261020_1611212 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72

Amesema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya Shandong Limited kutoka China kwa gharama ya Sh bilioni 124.6, chini ya usimamizi wa kampuni ya Lea kutoka India, huku ufadhili ukitolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Akizungumzia maendeleo ya ujenzi huo, Mhandisi Msama amesema kazi za msingi pamoja na ujenzi wa nguzo zote tisa za daraja hilo zimekamilika, huku ujenzi wa sehemu ya juu ya daraja (deck) ukiendelea kwa kutumia teknolojia ya Moving Scaffolding System (MSS).

1003465732 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72

Amesema teknolojia hiyo ni miongoni mwa mifumo inayotumika katika ujenzi wa madaraja, ikisaidia utekelezaji wa kazi za sehemu ya juu ya daraja kwa kutumia vifaa maalumu vya kisasa.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, kupunguza utegemezi wa vivuko, kuongeza fursa za biashara na kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii, hususan kwa wananchi wa Pangani, mkoa wa Tanga na maeneo mengine.

1003465754 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72

Mhandisi Msama aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huo, huku akitoa shukrani kwa Wizara ya Ujenzi na uongozi wa TANROADS kwa ushirikiano na usimamizi wa mradi.

1003465703-1 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72
1003465705 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72
1003465714 Ujenzi wa daraja la Pangani wafikia asilimia 72

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *