TMA yawagusa wenye mahitaji kushehekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANAWAKE wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa kufanya shughuli tofauti za kijamii zinazolenga kuimarisha mshikamano na kusaidia jamii.

Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi kufikia Dira ya Maendeleo 2050.”

Katika Mkoa wa Dodoma, watumishi wanawake wa TMA walipata fursa ya kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Safina kilichopo Ntyuka, ambapo walikutana na watoto wanaolelewa katika kituo hicho na kuwapa faraja pamoja na kuwasaidia kwa mahitaji mbalimbali.

Ziara hiyo ililenga kuonesha upendo, mshikamano na kuwapa matumaini watoto wasiokuwa na wazazi au wale wanaoishi katika mazingira magumu.

WhatsApp-Image-2026-03-08-at-12.02.08 TMA yawagusa wenye mahitaji kushehekea Siku ya Wanawake Duniani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *