Tanzania yatumia maonesho ya Paris kuvutia utalii

Paris, Ufaransa

Tanzania inashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya IFTM Top Resa 2026 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa, kuanzia Septemba 15 hadi 17, 2026.

1003071067-1024x576 Tanzania yatumia maonesho ya Paris kuvutia utalii

Maonesho hayo yanawakutanisha zaidi ya wataalamu 32,000 wa sekta ya utalii, bidhaa na taasisi 1,650 pamoja na maeneo 177 ya utalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa, ukiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Saidi Yakubu.

Katika maonesho hayo, Kamisheni ya Utalii Zanzibar inaongoza ujumbe wa kampuni 15 za Kitanzania, zikiwemo hoteli, mashirika ya ndege, kampuni za kuendesha shughuli za utalii na wadau wengine wa sekta hiyo.

1003071066-1024x683 Tanzania yatumia maonesho ya Paris kuvutia utalii

Ushiriki huo unatoa fursa muhimu kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake vya kipekee vya utalii kwa washiriki kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Aidha, maonesho hayo yanatoa fursa ya kujenga ushirikiano wa kibiashara pamoja na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika soko la utalii la kimataifa.

1003071068-1024x576 Tanzania yatumia maonesho ya Paris kuvutia utalii

Maonesho ya IFTM Top Resa 2026 yanaendelea jijini Paris hadi Septemba 17, yakikutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *