Tanroads yafanya tathmini ya km 2,071 za barabara, madaraja 1,032 kabla ya mvua

1003132006-1 Tanroads yafanya tathmini ya km 2,071 za barabara, madaraja 1,032 kabla ya mvua

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

WIZARA ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro umeimarisha ufuatiliaji wa hali ya barabara na madaraja katika mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa mvua za El-Nino.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Baraka Mwambage, amesema wataalamu wa wakala huo wamefanya tathmini ya mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 2,071 pamoja na madaraja 1,032, kwa lengo la kubaini maeneo yanayohitaji uangalizi wa karibu wakati wa msimu wa mvua.

1003131995 Tanroads yafanya tathmini ya km 2,071 za barabara, madaraja 1,032 kabla ya mvua



Amesema tathmini hiyo imeiwezesha TANROADS kubaini maeneo 49 yanayohitaji ufuatiliaji maalumu, hivyo kuweka mkazo katika maandalizi kulingana na hali na mahitaji ya maeneo hayo.

“Baada ya Serikali kutoa tahadhari ya El-Nino, tulifanya tathmini katika mtandao wetu wote na kubaini maeneo yanayohitaji uangalizi maalumu. Hatua hii inatusaidia kuelekeza ufuatiliaji na maandalizi yetu kwa wakati,” amesema Mhandisi Mwambage.

1003132012 Tanroads yafanya tathmini ya km 2,071 za barabara, madaraja 1,032 kabla ya mvua


Ameongeza kuwa TANROADS itaendelea kufuatilia hali ya barabara, madaraja na makalavati, pamoja na kuchukua hatua za tahadhari pale inapohitajika, ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua katika miundombinu hiyo.

Aidha, amewataka wananchi kutoa taarifa mapema wanapoona changamoto katika barabara, madaraja au makalavati, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.

MWISHO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *