TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia

WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.45-1-1024x682 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewataka wanaume na vijana wa kiume kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.

TAMWA imeeleza kuwa kundi hilo lina nafasi muhimu katika kubadili mitazamo na mienendo inayochochea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, ameyasema hayo jana Mei 8, 2026 jüjini Dar es Salaam wakati akizungumza katika mjadala uliowakutanisha wadau wa masuala ya ukatili wa kijinsia.

Amesema ni wakati sasa wa wanaume kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto hiyo badala ya kuonekana kama watazamaji.


Amesema kupitia mradi wa “Sauti Zetu” unaotekelezwa kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), TAMWA imeona umuhimu wa kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwamo wanafunzi, walimu, viongozi wa serikali, mashirika ya kijinsia pamoja na makundi ya wanawake kujadili nafasi ya wanaume katika kutokomeza ukatili wa kijinsia.


Dkt. Rose amesema tafiti zinaonyesha ukubwa wa tatizo hilo duniani ambapo kwa mujibu wa Benki ya Dunia mwaka 2019, asilimia 38 ya mauaji ya wanawake hufanywa na wapenzi wao wa karibu.


Aidha, amesema wanaume nao hukumbwa na ukatili hasa wa kihisia lakini wengi hushindwa kuripoti kutokana na hofu, aibu au kukosa mifumo rafiki ya kusaidia kundi hilo.

Katıka kampenı ya lAMWA inayohamasısha wanaume kushiriki kupinga ukatili wa kıjinsıa, Dkk Rose, amesema kampeni hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu kupitia shughuli za mashinani.


Amesema wanakutana moja kwa moja na wanafunzi wa shule
za msingi na sekondari, walimu, wazazi hasa akina mama pamoja na wadau wa elimu, ulinzi na usalama na viongozi wa mitaa na vijiji.

WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.46-3-1024x819 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia


Ameeleza kuwa kupitia mikutano hiyo hupata taarifa moja kwa moja kutoka kwa jamii kuhusu matukio ya ukatili yanayotokea kwenye mazingira yao, jambo linalosaidia kuandaa taarifa sahihi na kuelimisha jamii kupitia vyombo vya habari.


Amesisitiza kuwa licha ya kampeni kufanyika katika maeneo
machache, imekuwa na matokeo makubwa kutokana na usambazaji wa taarifa kupitia vyombo vya habari.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), Agnes Mwafifi, amesema wanaume wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, kwa kuwa bado wapo katika nafasi nyingi za uongozi ndani ya jamii.

“GIZ kwa kushirikiana na TAMWA tunatumaini kupitia mdahalo huu wanaume watasimama imara katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kuanzia sasa,” amesisitiza.

Naye Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Ubungo Beatrice Mbawala amesema mabadiliko makubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia yanaweza kupatikana ikiwa wanaume watapewa nafasi na kipaumbele katika kupinga vitendo hivyo ndani ya jamii.

WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.47-1024x819 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia
WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.46-2-1024x819 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia
WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.45-1024x819 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia
WhatsApp-Image-2026-05-08-at-10.26.42-1024x819 TAMWA: Wanaume, wavulana wana mchango mkubwa vita dhidi ya ukatili wa kijinsia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *