
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mvua hizo zinatarahiwa kunyesha kwa siku tano kuanzia kesho Februari 27, 2026.
Katika taarifa iliyotolewa na TMA kwa vyombo vya habari leo Februari 26,2026, imeeleza kuwa wastani wa kiwango cha athari zinazowekea ni pamoja na baadhi ya maeneo kuzungukwa na maji.
Taarifa imeeleza kuwa, Februari 27, 2026, mvua kubwa zinatarajiwa kutokea kwa maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Iringa, Njombe na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha, Februari 28, 2026 mvua kubwa inatarajiwa kutokea kwa maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Machi Mosi angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Rukwa, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.