Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili

WhatsApp-Image-2026-03-24-at-01.57.56-1024x874 Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Serikali imeanza mazungumzo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja na uongozi wa Kampuni Mama inayomiliki Faceebok, Instagram na WhatsApp (META) ili Lugha ya Kiswahili itambulike rasmi kwenye Majukwaa ya Kimtandao na kuwezesha Vijana wanaotengeneza maudhui kwa lugha hiyo walipwe malipo makubwa kulingana na kazi zao.

Amesema hayo wakati wa Kongamano la 5 la Idhaa za Kiswahili duniani, lililofanyika jana Machi 24, 2026 jijini Arusha, ambapo amebainisha kuwa licha ya maudhui ya Lugha ya Kiswahili hususani ya Tanzania kuwa mazuri na kupata watazamaji wengi lakini warushaji maudhui hayo wanalipwa kidogo kutokana na lugha hiyo kutokuwa rasmi kwenye majukwaa ya mitandao hiyo ukilinganisha na Lugha ya Kiingereza,

“leo hii unamkuta Mtu wa Tanzania ana followers zaidi ya milioni 3, akipost wanaotazama ni wengi ila hapati pesa kupitia Instagram, Facebook, TikTok hawawalipi kwasababu kiswahili bado Watu wa META na wenye platform ya mitandao duniani hawajakitambua kama lugha rasmi” amesisitiza Makonda

WhatsApp-Image-2026-03-24-at-01.57.56-1-1024x638 Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili
WhatsApp-Image-2026-03-24-at-01.57.57-1024x638 Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili
WhatsApp-Image-2026-03-24-at-01.57.58-1024x834 Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili
WhatsApp-Image-2026-03-24-at-01.57.58-1-781x1024 Serikali yaanza mchakato kuwanufaisha watengeneza maudhui ya Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *