Serikali kupunguza kodi kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

WhatsApp-Image-2026-06-11-at-07.29.43-1024x683 Serikali kupunguza kodi kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imependekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mita janja za gesi ya mitungi ya kupikia (LPG Smart Meter) zinazoingizwa nchini katika hatua inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Pendekezo hilo limewasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Juni 11, 2026 na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Waziri Omar amesema hatua hiyo ni sehemu ya maboresho ya kodi yanayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi na mbadala katika vyombo vya moto na majumbani.

Mbali na msamaha huo, Serikali imeendelea kutoa vivutio mbalimbali vya kikodi katika sekta ya nishati safi ikiwemo msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani katika mnyororo wa uzalishaji wa Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG), vifaa vya kubadilisha magari kutoka matumizi ya mafuta kwenda matumizi ya gesi na umeme pamoja na malighafi zinazotumika kutengeneza mitungi ya gesi.

Hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini kupitia maboresho mbalimbali ya kikodi yaliyopendekezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

WhatsApp-Image-2026-06-11-at-07.29.43-1-1024x683 Serikali kupunguza kodi kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *