RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili mkoani Arusha leo na kupokelewa na viongozi mbalimbali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu pamoja pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Machi 6, 2026.
Rais Dkt. Samia amewasili Jijini Arusha kwaajili ya kushiriki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika Machi 7, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Alipowasili mkoani hapo pia amepokelewa na Kikundi cha Sanaa cha Maasarie Troupe kilichotoa burudani.








