NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma

1000959701-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma

Na Mwandishi Wetu, OR- TAMISEMI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Zainabu Katimba, amepokea vifaa vyenye thamani ya Sh. mil.42.4 kwaajili ya huduma za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha kwa jamii.

Akipokea vifaa hivyo, Katimba amesema serikali inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, elimu na miundombinu hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.

“Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwamo Afya na Elimu, ”amesema.

Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu Meneja wa NMB, Kanda ya Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, viti vitano (05) kwaajili ya wagonjwa, vitanda kumi (10) kwaajili ya wajawazito kujifungulia ambavyo vyote vimetolewa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda 50 kwa wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Hata hivyo, vifaa vya Afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha Afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.

1000959710-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma
1000959704-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma
1000959705-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma
1000959700-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma
1000959702-1024x682 NMB yakabidhi vifaa vya mil. 42.4 Kigoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *