Ndejembi atoa angalizo Ujenzi wa stendi ya Sh. bilioni 8.4 Namtumbo

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma

MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi, ametoa angalizo kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Namtumbo wenye thamani ya Sh bilioni 8.4, akishauri miradi inayotegemea fedha za maendeleo kutoka Serikali kutekelezwa kwa awamu ili kuongeza ufanisi na kutoa uhakika wa kukamilika kwa wakati.

Ametoa angalizo hilo leo Novemba 11, 2025, wakati akikagua mradi huo akiwa katika ziara ya mkoani Ruvuma, ambapo pia amepongeza jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo katika kusimamia utekelezaji wake.

1003708212-1024x683 Ndejembi atoa angalizo Ujenzi wa stendi ya Sh. bilioni 8.4 Namtumbo

Mradi huo ulianza kutekelezwa Oktoba 2026 na unatarajiwa kukamilika Septemba 2027 ambapo kwa sasa, mkandarasi wa mradi huo, kampuni ya AMJ Contractors Ltd, yuko katika hatua za awali za uchimbaji wa msingi.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi, Allen Mshiru, stendi hiyo itakuwa na maeneo ya kuegesha magari, fremu 197 za maduka, maeneo ya lami, jengo la utawala pamoja na kituo cha polisi.

1003708209-1024x682 Ndejembi atoa angalizo Ujenzi wa stendi ya Sh. bilioni 8.4 Namtumbo

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Ndejembi amesema Serikali tayari imetoa takribani Sh bilioni moja kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo, ambao unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi, kuongeza mapato ya halmashauri na kufungua fursa za ajira na biashara kwa vijana, wajasiriamali na mama lishe.

Katika mkutano huo, Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Profesa Riziki Shemdoe, amesema Serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 3.9 pamoja na daraja lenye thamani ya Sh bilioni 1.1 wilayani Namtumbo.

1003708216-1024x683 Ndejembi atoa angalizo Ujenzi wa stendi ya Sh. bilioni 8.4 Namtumbo
1003708208-1024x682 Ndejembi atoa angalizo Ujenzi wa stendi ya Sh. bilioni 8.4 Namtumbo

Makamu wa Rais ameelekeza barabara hizo ziwekwe taa baada ya kukamilika ili kuimarisha usalama na kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea wakati wa usiku.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kusimamia kwa karibu miradi yote ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wananchi wanapata huduma bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *