Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama

WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.25-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama

Na Mwandishi Wetu, Kahama

WANANCHI wa Manispaa ya Kahama wamepata faraja kubwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa umaliziaji wa miundombinu ya barabara na mitaro chini ya Mradi wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC).

Uzinduzi huo umefanyika Mei 27, 2026 na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe.

Waziri Shemdoe amesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya miji.

Mradi wa TACTIC, unaofadhiliwa kwa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 410 kutoka Benki ya Dunia, unatekelezwa katika miji 45 nchini, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa ukuaji wa miji na kuongeza uwezo wa Halmashauri kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa Manispaa ya Kahama, utekelezaji wa awamu ya kwanza ulianza Novemba 2023 kwa gharama ya Sh. bilioni 20.86, lakini ulipata changamoto kutokana na udhaifu wa mkandarasi wa awali.

Serikali ilichukua hatua za kisheria na hatimaye kusitisha mkataba huo.

Waziri Shemdoe ameeleza kuwa hatua hiyo ni funzo kwa wakandarasi wote, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia uzembe katika miradi ya maendeleo.

Amesema kwa sasa, kazi za viporo zitaendelezwa na Mkandarasi mpya, kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation, ambapo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati.

Awamu ya pili ya mradi kwa miji ya kundi la kwanza, ikiwamo Kahama, inahusisha ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi eneo la Mbulu, Soko Kuu la Sango, na kituo kidogo cha daladala pamoja na soko la wajasiriamali Zongomela.

Mkataba huu wenye thamani ya Sh. bilioni 27.43 ulianza kutekelezwa Desemba 2024 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2026.

Waziri Shemdoe amebainisha kuwa miradi hiyo italeta mabadiliko makubwa kwa wananchi wa Kahama na wageni, ikiwemo kuboresha huduma za usafiri na biashara, kuongeza thamani ya maeneo husika, na kuchangia mapato ya Halmashauri.

Aidha, ametoa maelekezo kwa wakandarasi kuhakikisha kazi inakamilika kwa ubora na muda uliopangwa, kwa washauri wa kitaalamu kusimamia kikamilifu mikataba, na kwa wakurugenzi wa Halmashauri kutumia rasilimali zilizopo kusimamia utekelezaji.

Wananchi wa Kahama wameonesha matumaini makubwa kuwa miradi hii itakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku ikibadilisha sura ya mji na kuufanya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika Kanda ya Ziwa.

WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.25-1-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.25-2-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.25-3-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.25-4-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.27-2-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.27-3-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.27-4-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.27-5-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama
WhatsApp-Image-2026-05-28-at-04.06.28-1024x683 Mradi wa TACTIC kubadili taswira ya Manispaa ya Kahama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *