Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika

WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.33-1024x777 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika

Na Mwandishi Wetu, Pwani

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza Kikao cha 12 cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambapo, pamoja na mambo mengine, vimejadili hali ya siasa, ukombozi wa kiuchumi na kuboresha hali za wananchi katika nchi zao.

Kikao hicho kilichofanyika leo Machi 5, 2026, Kibaha, mkoani Pwani, kilihusisha Makatibu Wakuu wa Vyama sita vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambavyo ni ANC (Afrika Kusini), CCM (Tanzania), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe) na MPLA (Angola).

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Asha-Rose Migiro, amesema kuwa katika kikao hicho wamepitia maazimio ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa vyama hivyo uliofanyika mwaka jana, nchini Afrika ya Kusini.

Alisema mijadala ilijikita kuangalia hali ya kisiasa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, hususan kulinda uhuru wa kisiasa na kiuchumi, kutathmini malengo ya harakati za ukombozi pamoja na kuendelea kulinda na kuimarisha uhuru uliopatikana.

Dkt. Migiro amesema jukumu kubwa la vyama hivyo ni kuimarisha mshikamano na umoja wao pamoja na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili kanda hiyo ikiwamo mabadiliko ya tabianchi. Aidha, walijadili namna ya kutatua migogoro katika nchi wanachama na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Katika kikao hicho pia walifanya mapitio ya maendeleo yaliyopatikana katika nchi zao, ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za jamii, kuboresha miundombinu pamoja na kuweka mikakati ya kujenga uchumi stahimilivu na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na umuhimu wa kuongeza ajira kwa vijana, kuwawezesha wanawake pamoja na kujenga uchumi jumuishi na stahimilivu kwa maendeleo ya Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.39-1-1024x782 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika
WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.39-1024x811 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika
WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.38-1024x590 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika
WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.37-1024x625 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika
WhatsApp-Image-2026-03-05-at-07.09.34-1024x512 Makatibu wakuu vyama vya ukombozi wajadili hali ya kisiasa kusini mwa Afrika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *