
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Mei 15, 2026 amewasili mkoani Mara kwa shughuli za Kikazi.
Pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki Mazishi ya Boniface Makene, aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, yatakayofanyika katika Kijiji cha Mabui, Musoma Vijijini mkoani Mara, kesho Mei 16, 2026.



