Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa

WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.07-1024x682 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Mazingira, Reuben Kwagilwa, ametembelea mabanda mbalimbali ya taasisi na wadau wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Kwagilwa amepata fursa ya kujionea shughuli, huduma na teknolojia mbalimbali zinazochangia uhifadhi wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za asili pamoja na juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa pongezi kwa taasisi na wadau wanaoshiriki maonesho hayo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira katika shughuli za kila siku.

Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wananchi ni muhimu katika kufanikisha juhudi za uhifadhi wa mazingira na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Taifa.

WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.07-1-1024x682 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa
WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.08-1024x682 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa
WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.09-1024x682 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa
WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.03-1024x682 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa
WhatsApp-Image-2026-06-01-at-07.46.01-1024x592 Kutunza mangira ni wajibu wa kila Mtanzania-Kwagilwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *