‘Kila la kheri wanangu wa kidato cha sita’

WhatsApp-Image-2026-05-04-at-03.03.17-1024x739 'Kila la kheri wanangu wa kidato cha sita'

“NINAWATAKIA kila la kheri wanangu wanafunzi wa Kidato cha Sita na Vyuo vya Ualimu kwa ngazi ya Cheti na Stashahada mlioanza mitihani yenu ya kuhitimu leo. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu wa akili na afya njema ili mfanye mitihani kwa uaminifu, kujiamini na mafanikio,” amesema Rais Samia leo Aprili 4, 2026 katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

ameongeza kuwa, “Serikali inaendelea kuwaandalia mazingira mazuri kwa hatua zinazofuata ikiwemo kuongeza mikopo na ufadhili wa masomo, kujenga vyuo vikuu katika kila mkoa na vyuo vya ufundi kila wilaya, na kuboresha mitaala ili elimu iwe bora na nafuu zaidi, iwawezeshe kujiajiri na iendane na mabadiliko ya dunia.”

Leo Aprili 4, 2026 wanafunzi wa kidato cha sita 133,655 kote nchini, wameanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari kwa mwaka 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *