JWTZ yaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani kimataifa-Dkt. Nyansaho

WhatsApp-Image-2026-05-19-at-02.22.03-1-1-1024x682 JWTZ yaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani kimataifa-Dkt. Nyansaho

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Rhimo Nyansaho, amesema Serikali kupitia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imeendelea kushirikiana na jumuiya za kimataifa na kikanda katika operesheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU).

Dkt. Nyansaho amesema hayo leo Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo.

Amesema kwa sasa JWTZ ina vikundi vya ulinzi wa amani vinavyotekeleza majukumu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Democratic kupitia operesheni ya MONUSCO, Jamhuri ya Afrika ya Kati kupitia MINUSCA pamoja na Lebanon kupitia UNIFIL.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, hali ya usalama kwa vikundi vyote vya JWTZ vinavyoshiriki operesheni hizo ni shwari na vinaendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa katika kulinda amani na usalama wa kimataifa.

Aidha, amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kuboresha hali ya zana na vifaa vya JWTZ pamoja na vikundi vinavyoshiriki katika operesheni za ulinzi wa amani ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa kiwango cha kimataifa.

WhatsApp-Image-2026-05-19-at-02.22.07-1024x683 JWTZ yaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani kimataifa-Dkt. Nyansaho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *