Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS

WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.28-1024x743 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Adam Joseph Mrisho ambaye amefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika Machi 23, 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. James Kilabuko pamoja na Mratibu wa Masuala ya UKIMWI, Adela Mpina.

Dkt.Yonazi ameahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.

WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.29-1024x683 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS
WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.29-1-1024x1006 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS
WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.30-1024x683 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS
WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.31-1-1024x683 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS
WhatsApp-Image-2026-03-23-at-03.09.32-1024x890 Dkt. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TACAIDS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *