
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Bandari ya Dar es Salaam inahudumia wastani wa tani milioni 1.6 ya mizigo kutoka nchini Rwanda, sawa na takriban asilimia 70 ya mizigo yote ya Taifa hilo.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo, Jumapili Mei 3, 2026 alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikao chake cha uwili na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aliyakuja nchini kwa ziara ya siku moja.
“Kama nchi yenye bandari, tuna wajibu wa kuhakikisha nchi zisizo na bandari zinahudumiwa kwa ufanisi. Tumekubaliana kuboresha zaidi huduma bandarini na kuweka mifumo maalumu ya kurahisisha mizigo ya Rwanda,” amesema.




