Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo

WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.17-1024x576 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Kamishna wa Ardhi kuongoza mwenyewe kliniki ya kusikiliza na kushughulikia kero za ardhi za wananchi wa Bagamoyo kuanzia Jumatatu ijayo.

Ameelekeza afike na timu kutoka makao makuu, ikishirikiana na wataalamu wa mkoa, Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kufanya kazi wiki nzima.

Ametoa maelekezo hayo leo, Ijumaa, Oktoba 16, 2026, alipozungumza na wananchi mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja.

“Usitume mwakilishi, uje mwenyewe kusikiliza mtu mmoja mmoja wewe mwenyewe,” amesema.

Dkt. Mwigulu amesema migogoro ya ardhi inahatarisha undugu na mshikamano, na tayari amewaelekeza Waziri wa Ardhi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri anayesimamia TAMISEMI kupitia upya utaratibu wa kuitatua. Aidha, amesisitiza wananchi wanaopisha uwekezaji na miradi ya maendeleo walipwe fidia stahiki bila kupunjwa.

Kuhusu huduma za afya, amekataza kuwachangisha wananchi fedha za mafuta ya magari ya kubebea wagonjwa wanaopelekwa hospitali za rufaa, akisisitiza kuwa mamlaka zinazoyasimamia zinapaswa kuhakikisha yana mafuta na yanatoa huduma iliyokusudiwa.

Pia, amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutokuzuia miili ya marehemu hospitalini kutokana na madai ya malipo. Amevielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia ununuzi, usambazaji na matumizi ya dawa za serikali ili kuhakikisha zinawafikia wananchi.

Waziri Mkuu amesema sekta binafsi imara na viwanda vya kuchakata mazao ni muhimu katika kuongeza ajira na kipato. Amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji na uzalishaji, huku akisisitiza matumizi bora ya ardhi na uzingatiaji wa sheria.

WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.18-1024x576 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo
WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.19-1024x576 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo
WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.22-1024x576 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo
WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.25-1024x576 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo
WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.26-1024x682 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo
WhatsApp-Image-2026-10-16-at-08.00.27-1024x541 Dkt. Mwigulu Aagiza Hati ya Kurasimisha Hadhi ya Bagamoyo Ipatikane Wiki Ijayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *