Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora

Na Mwandishi Wetu, Iringa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Jumatatu,Machi 9,2026, amefungua rasmi mafunzo maalum ya uongozi na utawala bora kwa viongozi na watendaji waandamizi wa chama yanayofanyika katika Ukumbi wa Mount Royal, Mkoani Iringa.

Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Jitegemee Holdings Company Limited (JHCL) kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), na yanawaleta pamoja wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya Jitegemee Holdings pamoja na viongozi waandamizi wa CCM.

Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Migiro amesema kuwa uongozi na utawala bora ni msingi muhimu wa kuimarisha taasisi na kuendeleza maendeleo ya Taifa, akisisitiza kuwa mafunzo hayo yanaendana na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 pamoja na maono ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, amewataka washiriki kutumia fursa ya mafunzo hayo kujenga uwezo wa kiuongozi na kuhakikisha maarifa watakayopata yanatumika kuimarisha utendaji wa taasisi wanazoziongoza.

WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.13-1024x688 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.14-1024x682 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.15-1024x664 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.16-1024x570 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.17-1-1024x790 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.20-1024x633 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora
WhatsApp-Image-2026-03-09-at-06.53.21-1024x578 Dkt. Migiro afungua mafunzo ya uongozi na utawala bora

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *