Dar yaendelea kung’ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENGE wa Uhuru 2026 unaendelea kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo Wilaya ya Kigamboni miradi 6 yenye thamani Sh. bil. 19.4 imepitiwa na Mwenge na hakuna uliokataliwa.

Aidha, katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru 2026 umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama, kikundi cha vijana Suluhu na Mipango kinachojishughulisha na usafilishaji wa abiria, ujenzi wa barabara ya Lingia- Nyakwale kwa kiwango cha lami na zege Km 3.7, mradi wa usambazaji maji kigamboni loti III, ujenzi wa nyumba ya watumishi kituo cha afya Tundwi Songani, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, matundu 10 ya vyoo na kichomea taka Shule ya Sekondari Kibugumo na ujenzi wa Hospitali ya Qualitas Kigamboni.

Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 15,2026 umeendelea Wilaya Temeke ambapo umekagua na kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

WhatsApp-Image-2026-04-14-at-23.36.02-1024x751 Dar yaendelea kung'ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026
WhatsApp-Image-2026-04-14-at-23.36.03-1024x837 Dar yaendelea kung'ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026
WhatsApp-Image-2026-04-14-at-23.36.03-1-1024x682 Dar yaendelea kung'ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026
WhatsApp-Image-2026-04-14-at-23.36.01-1024x683 Dar yaendelea kung'ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026
WhatsApp-Image-2026-04-14-at-23.36.00-1024x785 Dar yaendelea kung'ara mbio za Mwenge wa Uhuru 2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *