CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BENKI ya CRDB imetoa wito kwa waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha jamii na kubadili mitazamo ya wananchi kuhusu matumizi ya majiko banifu, ikieleza kuwa baadhi ya changamoto zinazokwamisha matumizi yake zinatokana na imani na tamaduni zilizojengeka katika jamii.

Meneja wa Sera na Mikakati Uendelevu kutoka CRDB, Rukonge Sospeter Muhongo ameyasema hayo leo Novemba 13, 2026 kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (Dar -PC), wakati akiwasilisha mada inayohusu nafasi ya Benki hiyo katikati kuwezeshwa matumizi ya teknolojia na mifumo ya kidigitali katikati kukuza Nishati safi yakupikia.

1003737251-1024x768 CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Amesema matumizi ya majiko banifu yanahusisha masuala ya kitamaduni yanayohitaji elimu ili wananchi waweze kuyakubali na kuyatumia.

Amesema baadhi ya wananchi wanaamini kuwa vyakula kama wali wa nazi haviwezi kuwa vitamu vinapoandaliwa kwa kutumia majiko banifu, hali inayodhihirisha umuhimu wa kutoa elimu kuhusu teknolojia hizo.

Muhongo amesema waandishi wa habari wana nafasi muhimu katika kubadili fikra hizo kwa kuandaa habari zinazowaeleza wananchi manufaa ya majiko banifu, aina zake, ubora, teknolojia zinazotumika na muda ambao yanaweza kudumu.

1003737262-1024x768 CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Amesema mbali na manufaa yake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kupunguza ukataji wa miti na kusaidia watoto kubaki shuleni, matumizi ya majiko banifu pia ni fursa ya biashara kwa wajasiriamali wadogo na wadau wengine wanaoshiriki katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji na matumizi yake.

Akieleza hatua zinazochukuliwa na CRDB katika kuunga mkono ajenda ya nishati safi ya kupikia, amesema benki hiyo imeanzisha mpango wa Kijani Bond na kuweka fedha takribani Dola za Marekani milioni 62, sawa na Sh bilioni 157.1, kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na ufadhili na uendeshaji wa sekta hiyo.

1003739657-1-1024x683 CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Amesema bidhaa za nishati safi ya kupikia ni sehemu muhimu ya mpango huo, ambapo benki hiyo pia ikiandaa bidhaa mpya zitakazounganisha biashara ya hewa ukaa na matumizi ya majiko banifu ili fedha zitakazopatikana ziweze kunufaisha jamii na wadau wa mnyororo wa thamani.

1003737008-1024x683 CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Ameongeza kuwa CRDB Bank Corp na Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), kilicho chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, vinatarajiwa kusaini mkataba unaohusu bidhaa ya biashara ya hewa ukaa na namna ya kutumia fursa hiyo kupitia majiko banifu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Bakari Kimwanga amesema wanahabari bado wana kazi kubwa ya kuendelea kuifanyia taifa kupitia taarifa zinazosaidia jamii kuelewa changamoto zake na kutafuta suluhisho.

1003734216-1024x683 CRDB yataka mabadiliko ya mitazamo kuhusu majiko banifu

Amesema Dar PC itaendelea kujivunia nafasi ya wanahabari katika kulisaidia taifa kupitia taarifa zenye manufaa kwa jamii na zinazowapa wananchi nafasi ya kusikika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *