Bei ya mafuta yaendelea kushuka

WhatsApp-Image-2026-09-01-at-13.48.49-1024x683 Bei ya mafuta yaendelea kushuka

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2026.

Bei ya petroli imeshuka kwa Sh. 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa Sh.101 kwa lita. Bei hizo zitaanza kutumika kuanzia Septemba 2, 2026, saa 6:01 usiku.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na EWURA, inaeleza kuwa, inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia.

“Mabadiliko ya bei yanaendelea kuathiriwa pamoja na mambo mengine na hali ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015, bei za mafuta zinaendelea kupangwa kwa kuzingatia mfumo wa soko. wafanyabiashara wote wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zisizozidi bei elekezi na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa EWURA kwa kituo chochote cha mafuta kitakachouza zaidi ya bei elekezi.

WhatsApp-Image-2026-09-01-at-13.48.53-1024x682 Bei ya mafuta yaendelea kushuka
WhatsApp-Image-2026-09-01-at-13.48.52-682x1024 Bei ya mafuta yaendelea kushuka
WhatsApp-Image-2026-09-01-at-13.48.52-1 Bei ya mafuta yaendelea kushuka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *