PPP muhimu viwanda vya dawa nchini-TPMA

WhatsApp-Image-2026-06-08-at-06.40.31-1024x1024 PPP muhimu viwanda vya dawa nchini-TPMA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CHAMA cha Wamiliki wa Viwanda vya Dawa Tanzania (TPMA), kupitia kwa mwenyekiti wake ambaye pia ni mwekezaji wa ndani kwenye sekta ya afya, Bashiru Haroon, kimeishauri Serikali kutengeneza sera shirikishi zitakazoondoa vikwazo vya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, hususan katika maeneo nyeti ya afya na elimu.

Haroon ametoa msimamo huo wa kimantiki, wakati akichangia mada katika Kongamano la Kitaifa la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) lililolenga kuleta mageuzi katika Sekta ya Afya nchini lililofanyika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), jijini Dar es Salaam.

Ameipongeza Serikali kwa hatua kubwa zilizofikiwa hadi sasa, Haroon amebainisha takwimu zinazoonyesha uhalisia wa uwekezaji.

Pia ameeleza kuwa kiwango cha uzalishaji wa dawa za ndani kimefikia asilimia 20, lakini akatoa matumaini makubwa kuwa, kwa kutumia sekta binafsi kwa njia ya PPP Tanzania inaweza kuzalisha kiwango kikubwa cha mahitaji yake ya dawa na vifaa tiba.

Hata hivyo, Haroon ameongeza kuwa, kufikia huo ni muhimu serikali na sekta binafsi kuwa na mtazamo wa pamoja kuhakikisha sekta hizo mbili zinaweka mkakati wa pamoja ili kubaini fursa na changamoto.

WhatsApp-Image-2026-06-08-at-06.40.31-1-1024x1024 PPP muhimu viwanda vya dawa nchini-TPMA
WhatsApp-Image-2026-06-08-at-06.40.31-2-1024x683 PPP muhimu viwanda vya dawa nchini-TPMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *