NEW YORK, Marekani
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Marekani, Megan Rapinoe, ni miongoni mwa nyota waliopata mafanikio katika kizazi chao, ametangaza kustaafu mwishoni mwa msimu huu.
Mshindi huyo wa Tuzo ya Ballon d’Or 2019, aliweka wazi hilo kabla ya kwenda kucheza fainali zake za nne za Wanawake za Kombe la Dunia, michuano itakayofanyika nchini Australia na New Zealand.
“Ninataka kufanya hili katika njia yangu binafsi,” amesema nyota huyo, 38.
“Ninajisikia fahari leo kuwa hapa na nimekuwa nikiaminika katika timu hii na mwili wangu umeshindwa kuendelea kwa muda mrefu.”
Nyota huyo ametwaa Kombe la Dunia mara mbili, atastaafu mwishoni mwa msimu akiwa na kikosi cha OL Reign kinachocheza NWSL, ambapo msimu wa kawaida unamalizika Oktoba na kucheza fainali ya mtoano Novemba.