Rais PSG amchimba ‘mkwara’ Mbappe

PARIS, Ufaransa

STRAIKA Kylian Mbappe, anatakiwa kusaini mkataba mpya endapo kama anataka kuendelea kubaki ndani ya Paris St-Germain, Rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi, amesema.

Al-Khelaifi ametoa kauli hiyo katika mkutano na Waandishi wa Habari wakati akimtambulisha Kocha mpya wa klabu hiyo, Luis Enrique siku chache baada ya kumtimua Christophe Galtier.

Straika huyo, 24 wa kimataifa wa Ufaransa, aliiambia PSG hatoongeza mkataba zaidi ya ule aliokuwa nao unaomalizika 2024.

“Lengo letu lipo wazi,” amesema Al-Khelaifi.

“Endapo Kylian Mbappe akitaka kubakia, tutataka abakie, anatakiwa kusaini mkataba mpya.

“Hatutaweza kumuachia mchezaji bora ulimwenguni aondoke bure kwa sasa. Hilo haliwezekani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *