
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Adam Joseph Mrisho ambaye amefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikao hicho kimefanyika Machi 23, 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. James Kilabuko pamoja na Mratibu wa Masuala ya UKIMWI, Adela Mpina.
Dkt.Yonazi ameahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.




