CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

WhatsApp-Image-2026-03-06-at-03.48.34-1-1024x742 CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO, (Msumbiji), Ndugu Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, ambaye ameanza ziara rasmi ya kikazi kwa siku mbili nchini.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Machi 6, 2026, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, vyama hivyo viwili ambavyo vina urafiki na udugu wa kihistoria, vimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili, hasa kushirikiana kiuchumi.

WhatsApp-Image-2026-03-06-at-03.48.31-1024x827 CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
WhatsApp-Image-2026-03-06-at-03.48.32-1024x643 CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
WhatsApp-Image-2026-03-06-at-03.48.33-1024x563 CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi
WhatsApp-Image-2026-03-06-at-03.48.34-1024x589 CCM, Frelimo kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *