ANTALYA, Uturuki.
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili katika Jiji la Antalya, nchini Uturuki, leo Novemba 10, 2026, kushiriki Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).
Rais Samia amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Antalya, ambako anatarajiwa kuungana na viongozi wengine kujadili hatua za kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kupitia taarifa yake, Rais Samia amesema pamoja na kushiriki mkutano huo, anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan.
Aidha, amesema atahutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali na kushiriki kikao cha ngazi ya juu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika.

Amesema Tanzania inashiriki mkutano huo ikiongozwa na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yanayolenga kujenga Taifa linalozingatia uhifadhi wa mazingira na kustahimili mabadiliko ya tabianchi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.