Rais TNCC ahamasisha Kilimo cha kisasa cha mhogo

*Atoa Milioni 10/-ujenzi wa Kanisa

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

Rais wa Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Chemba za Biashara za Afrika (PACCI), Vicent Minja, ametoa Sh milioni 10 kuchangia ujenzi wa Kanisa Parokia ya Teule, Mwilamvya mkoani Kigoma, huku akiwahimiza wananchi kuwekeza katika kilimo cha kisasa cha mhogo kutokana na fursa zake katika masoko ya kimataifa.

Mchango huo umetolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo iliyokusanya takribani Sh milioni 137.

1003672812-1024x680 Rais TNCC ahamasisha Kilimo cha kisasa cha mhogo

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya harambee hiyo, Minja amesema ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za kijamii ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuchochea maendeleo ya jamii.

Amesema zao la mhogo lina fursa kubwa za kibiashara kutokana na kuongezeka kwa mahitaji yake katika masoko ya kimataifa, hususan nchini China, hivyo kuwataka wananchi na waumini kutumia fursa hiyo kwa kujikita katika kilimo cha kisasa.

1003672800-1024x680 Rais TNCC ahamasisha Kilimo cha kisasa cha mhogo

Mbali na mhogo, Minja amewahimiza wananchi kuongeza uzalishaji wa mazao mengine yenye fursa za kibiashara, yakiwemo mahindi na asali, kwa kuzingatia mbinu bora za uzalishaji, uchakataji na kuongeza thamani ili kunufaika na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amewataka pia viongozi wa dini kutumia nafasi zao kuwahamasisha waumini kujikita katika shughuli za kilimo na ufugaji nyuki kama njia ya kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.

1003672802-1024x680 Rais TNCC ahamasisha Kilimo cha kisasa cha mhogo

Amesema TNCC iko tayari kushirikiana na wakulima pamoja na wadau wengine wa sekta binafsi kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi, sambamba na kuwezesha upatikanaji wa fursa za biashara zitakazosaidia kuongeza kipato na kuchochea maendeleo ya jamii.

Minja amesisitiza kuwa ushiriki katika shughuli za kijamii ukiambatana na uwekezaji katika shughuli za uzalishaji mali, ikiwemo kilimo, ni sehemu muhimu ya kujenga uchumi imara na kuboresha maisha ya wananchi.

1003672795-1024x680 Rais TNCC ahamasisha Kilimo cha kisasa cha mhogo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *