Ten Hag akoshwa na Fernandes

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag, amemwagia sifa nahodha wake, Bruno Fernandes kutokana na kiwango alichokionesha baada ya mreno huyo kufunga bao la ushindi wakitoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Nottingham Forest uwanjani Old Trafford.

Ten Hag alisifia uongozi wa Fernandes licha ya kukosolewa na baadhi ya wachambuzi, akiwemo Micah Richards, kuwa kiungo huyo, 28, ana hasira sana kuwa nahodha mzuri.

Kocha huyo wa Kiholanzi amesifia kiwangobora cha kiungo huyo wakati United ikipambana kushinda licha ya kufungwa mabao mawili ndani ya dakika nne.

Katika mchezo huo, Fernandes alitoa pasi ya bao kwa Casemiro kabla ya kufunga la bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti baada ya Marcus Rashford kuchezewa faulo na Danilo.

“Kwa dhana yoyote, amecheza vizuri sana katika kiwango cha juu,” amesema Ten Hag.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *